# bustani ya Edeni "bustani iliyokuwa Edeni" # kuilima "kuilima". Hii ina maana ya kufanya kila kitu cha muhimu ili mimea iweze kuota vizuri. # kuitunza kuilinda dhidi ya mambo mabaya yanayoweza kuikuta # kutoka kwenye kila mti bustanini "Tunda katika kila mti la bustani" # wewe kiwakilishi ni cha kipekee # waweza kula kwa uhuru ...usile Katika baadhi ya lugha ni kawaida kusema kile ambacho hakiruhusiwi na kisha kusema kile ambacho hakiruhusiwi. # waweza kula kwa uhuru "waweza kula bila kizuizi" # mti wa ujuzi wa mema na mabaya "mti unaowapa watu uwezo wa kuelewa mema na mabaya" au "mti unaowafanya watu wanaokula matunda yake kujua mambo mazuri na mambo mabaya. # usile "sitakuruhusu ule" au "haupaswi kula"