# sentensi Unganishi Paulo alifundisha waamini jinsi wanavyopaswa kuwatendea waamini na jinsi Mungu anavyowapa thawabu. # Ndugu Lina maana ya jamaa ya Wakristo ikijumuisha kwa pamoja wanaume na wanawake, kwa kuwa waamini wote ndani ya Kristo ni wana familia moja ya kiroho na Mungu akiwa Baba yao wa mbinguni. # Ikiwa mtu "ikiwa mtu mmoja" au "mtu mmoja wapo miongoni mwenu" # amekamatwa katika makosa/dhambi Maana zinazokubalika hapa ni 1) mtu amepatikana katika tendo, " amekamatwa katika kitendo cha dhambi," au 2) mtu amefanya dhambi bila kudhamiria kufanya uovu," ''amefanya dhambi." # ninyi mlio wa kiroho "wale wanaoongozwa na Roho" au " ninyi mnaoishi chini ya uongozi wa Roho" # mrejeshe huyo mtu "msahihishe huyo mtu aliyefanya dhambi" au "mtie moyo aliyefanya dhambi aweze kurudia mahusiano sahihi na Mungu." # katika roho ya upole Maana zinazokubalika 1) Roho anamwelekeza mtu mwenye kutoa masahihisho au 2)" kwa mtazamo wa upole" au kwa njia ya upole" au "kwa hali ya uzuri". # Huku ukijiangalia mwenyewe maneno haya yanahusu Wagalatia kana kwamba ni mtu mmoja, lengo ni kutilia mkazo kwamba anaongea na mtu mmoja binafsi. "Jiangalie binafsi" au "ninamwambia kila mmoja wenu" "Jiangalie mwenyewe" # ili msijaribiwe Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. ''ili kwamba kisiwepo kitu cha kuwajaribu ninyi kutenda dhambi"