# Sentensi Unganishi: Paulo anawaambia waumini kwamba Wayahudi wanaojua sheria na Wamataifa ambao hawaijui sheria, wameokolewa kwa imani peke yake ndani ya Kristo na siyo kwa kutunza sheria. # si watu wa mataifa wenye dhambi "siyo wale watu wa mataifa ambao wayahudi huwaita wenye dhambi" # Tulikuja katika imani ndani ya Kristo Yesu "Tuliamini katika Kristo Yesu" # sisi Huenda pengine hii inamrejelea Paulo na wengine, na si Wagalatia. # hakuna mwili Neno mwili limetumika kuwakilisha mtu yaani "hakuna mtu"