# Sentensi Unganishi: Paulo anatoa sababu yake ya kuandika barua hii-anawakumbusha kuendelea kuielewa injili. # Ninashangaa "Ninashangazwa" au "Nimeshitushwa." Paulo alisikitishwa na mambo haya waliyokuwa wanayafanya. # kwamba mmegeuka haraka sana kutoka kwake... na kwenda kwenye injili nyingine Maana nyingine zaweza kuwa ni 1) " Mmeacha kwa haraka sana kumtumaini Yeye au 2) "mmeacha kwa haraka sana kuwa waaminifu kwake." # Yeye aliyewaita "Mungu, aliyewaita ninyi" # kuitwa Hapa inamanisha Mungu amewateua or kuwachagua watu kuwa watoto wake, kumtumikia na kuutangaza wa ujumbe wa wokovu kupitia kwa Yesu. # kwa neema ya Kristo " kwa sababu ya neema ya Krsto" au "kwa sababu ya dhabihu ya neema ya Kristo" # Mnageukia injili nyingine Mnaamini injili nyingine # watu watu wote au binadamu