# Maelezo ya Jumla: Huu ni mwendelezo wa ujumbe wa Yahwe kwa milima ya Israeli. # mtachipuza matawi na kuzaa matunda "miti yenu itachipuza matawi na kuzaa matunda." # tazama Neno "tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata." # nipo kwa ajili yenu "nataka kufanya mambo mazuri kwenu" Neno "ninyi" linarejea kwa milima ya Israeli. # na ninawatenda kwa fadhili "nitakuwa mkarimu kwenu" (UDB) # mtalimwa na kupandwa mbegu "Watu wangu, watalima aridhi yako na kuipanda mbegu." Kulima inamaanisha kukata matuta katika aridhi ili kupanda mbegu katika hiyo.