# Maelezo ya Jumla: Yahwe anaendelea kunena na Farao na kumfananisha na jitu la kutisha liishilo katika maji. # Bwana Yahwe asema hivi Tazama tafsiri yake katika sura ya 5:5. # Basi nitautandaza wavu wangu juu yako katika kusanyiko la watu wengi "Basi nitawakusanya watu wengi na kutupa wavu wangu juu yako." # watawainua juu katika wavu wangu "kutumia wavu wangu, watu watakuvuta kutokakwenye maji" # Nitakuacha katika nchi "Nitakuacha bila msaada katika nchi." Jitu la kutisha lililokuwa linatisha wakati lilipokuwa ndani ya maji haliwezi kufanya chochote wakati likiachwa juu ya nchi kavu. # ndege wote wa angani "ndege wote warukao katika anga" # njaa ya wanyama wote waishio juu ya nchi watashibishwa na wewe "nitawaacha wanyama wote wa nchi wataula mwili wako hadi njaa iwaishe"