# Maelezo ya Jumla: Yahwe anaendelea kumpatia Ezekieli ujumbe wake kwa wazee wa Israeli. # Kisha niliwapa amri ambazo hazikuwa nzuri, na maagizo ambayo hawakuweza kuishi kwayo Maneno amri katika hili neno halirejelei sheria ya Mungu. Mungu aliwaruhusu kuishi kwa sheria ya mwanadamu na hukumu ambazo hazikuwa nzuri. # kuwapatia Neno "wao" linarejea kwa watoto ambao Yahwe aliwatoa Misri. # kwa zawadi zao "kwa zawadi ambazo walizokuwa wamenipatia." # waweke kwenye moto Hii inamaanisha kutoa sadaka mtoto kwa sanamu kwa kuwachoma wakiwa hai.