# Taarifa za Msingi: Yehova anaendelea kuzungumza juu ya mwana asiyetenda dhambi kama za baba yake. # walio uchi Hii inaweza kumaanisha watu wasio na nguo kabisa, lakini kwa sehemu kubwa inamaanisha watu wenye mavazi chakavu, mavazi duni sana. # huwavika nguo walio uchi Kuwapatia nguo watu wenye uhitaji wa nguo linazungumziwa kama tendo la kuwavalisha nguo katika miili yao. (lugha ya picha) # huuondoa mkono wake kwa maskini Hapa neno "mkono" linasimama badala ya maneno "kutenda matendo yasiyo haki"