# ukoo wa kifalme Neno "ukoo wa kifalme" linawaelezea watu na vitu ambavyo vinavyohusiana na mfalme au malkia. # uzao, muundo wa uzao "Uzao" ni mtu mwenye uhusiano wa damu moja kwa moja toka kwa mtu mwingine wa mbali katika historia ya familia fulani. # agano Agano ni makubaliano rasmi, yenye ahadi za viapo baina ya pande mbili ambapo upande mmoja au pande zote zinalazimika kulitimiza. # nadhiri, kiapo, kujiapiza Katika Biblia, nadhiri ni ahadi rasmi ya kufanya jambo fulani. Mtu anayefanya nadhiri hutakiwa kuitimiza ahadi hiyo. Nadhiri inahusisha mtu kujitoa kuwa mwaminifu na mkweli.