# Maelezo ya Jumla: Yahwe anaendelea kunena na Ezekieli. # Bwana Yahwe Jina halisi la Mungu wa Kweli alilojifunua kwa wa Israeli. # Piga makofi na kanyaga kwa mguu wako Ezekieli alikuwa afanye hili tendo la ishara kupata umakini wa watu. Hii haikuwa makofi. # Ole Neno "Ole" limetumika kuelezea huzuni. # nyumba ya Israeli Neno "nyumba" ni mfano kwa ajili ya familia iishiyo katika nyumba, katika kesi hii Waisraeli, uzao wa Yakobo zaidi ya miaka mingi. "kundi la watu wa Israeli" # Kwa kuwa wataanguka kwa upanga, njaa, na tauni. "Kwa kuwa watakufa kwa upanga, njaa, na tauni." "Upanga", "njaa", na "tauni" ni njia mbali mbali watakazokufa. Upanga "upanga" inawakilisha vita. # nitaikamilisha ghadhabu yangu juu yao "nitatosheleza hasira yangu juu yao"