# Maelezo ya Jumla Yahweh anaendelea kuongea na Musa jinsi maskani itengenezwe. # Nawe fanya Yahweh anazungumza na Musa, hivyo neno "nawe" la muhusu yeye. Yahweh inawezekana alitarajia Musa kumwambia mtu mwingine kufanya kazi, lakini Musa atakuwa ana wajibika kuona kuwa kazi imefanywa sahihi. # vifungo Vifungo vintoshea kwenye tanzi kushikilia pazia pamoja. # nawe lete lile sanduku la ushuhuda Sanduku la agano ni chombo linalo hifadhi amri. # Lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu Hii yaweza andikwa katika tensi tendaji.