# Modekai Modekai alikuwa mwanamme myahudi akiishi katika nchi ya Waajemi. Alikuwa mlezi wa binamu yake Esta, ambaye baadaye alikuwa mke wa mfalme wa Uajemi, Ahausiero. # Muyahudi, Wayahudi Wayahudi ni uzao wa mjukuu wa Abrahamu, Yakobo. Neno Yahudi linatokana na neno Yuda. # lango, komeo "lango" ni kizuizi kilichowekwa mahali pa kuingilia katika fensi au ukuta unaozunguka nyumba.Komeo inamaanisha ubao au chuma ambacho kinaweza kusogezwa katika sehemu ili kufunga lango. # tangaza, mbiu ni kutangaza au kutangaza kitu kwenye hadhara na kwa ujasiri.