# Kwa maana ni kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani Wema wake Mungu kwetu ni sababu iliyotuwezesha sisi kuokolewa kutoka katika hukumu kama tu tutamwamini Yesu. # Haitokani na Neno "haitokani" linahusu au linarejea kwamba "kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani" # ...kutoka kwetu Neno "kwetu" linaelezewa kumaanisha Paulo na waamini wote katika Efeso. # sisi tu kazi ya Mungu Neno "sisi" linaelezewa kumaanisha Paulo na waamini wote katika Efeso # katika Yesu Kristo "Ndani ya Kristo" na maelezo kama hayo ni mifano ambayo mara nyingi hutokea katika barua au nyaraka za Agano Jipya. Inaelezea aina nzito kabisa ya mahusiano inayoweza kuwepo kati ya Kristo na wote wanaomwamini.