# Yeyote autazamaye upepo yawezekana asipande Maana zinazowezekana ni 1) "Mkulima yeyote anayetilia maanani upepo hatapanda wakati upepo unapopuliza upande usiofaa" au 2) "Mkulima yeyote anayetilia maanani sana upepo hatapanda." # yeyote atazamaye mawingu yawezekana asivune Maana zinazowezekana ni 1) "Mkulima yeyote anayetilia maanani mawingu hatavuna inapotaka kunyesha" au 2) "Mkulima yeyote anayetilia maanani sana mawingu hatavuna." # ambavyo mifupa ya mtoto ikuavyo Maana zinazowezekana ni 1) "jinsi mtoto anavyokuwa" au 2) "jinsi mifupa ya mtoto inavyokua."