# Ole wako ardhi ... umebarikiwa ardhi Katika mstari huu, mwandishi anazungumza na taifa kana kwamba ni mtu. # kama mfalme wako ni kijana mdogo Hii inamaanisha kuwa mfalme hana uzoefu au hajapevuka kiakili. Lakini tafsiri zingine za kisasa zinatafsiri neno la Kihebrania kama "mtumishi" # huanza karamu ahsubuhi Hii huashiria kuwa viongozi wanajali zaidi kuwa na wakati mzuri kuliko kuongoza taifa. # mfalme wako ni mwana wa waungwana Hii huashiria kuwa mwana huyu amefundishwa vizuri na wakubwa wake katika desturi za kuwa mfalme mzuri.