# Kama nzi walio kufa ... hivyo hivyo upumbavu kidogo Kama vile ambavyo nzi wanaweza kuharibu manukato, vivyo hivyo upumbavu unaweza kuharibu sifa ya mtu kwa hekima na heshima. # Moyo wa mtu mwenye hekima ... moyo wa mpumbavu Hapa neno "moyo" inamaanisha akili na nia. "Jinsi mtu mwenye hekima anavyowaza ... jinsi mpumbavu anavyowaza" # huelekea kulia ... huelekea kushoto Hapa maneno "kulia" na "kushoto" yanamaanisha yalio sawa na yasiyo sawa. "hufanya yaliyo sawa .. hufanya yasiyo sawa" # fikira zake zina upungufu "ni mjinga"