# mwanamke yeyote ambaye moyo wake umejaa mitego na nyavu, na ambaye mikono yake ni minyororo Mwandishi anasema mwanamke mshawishi ni kama mitego ambayo mwindaji anatumia kushika wanyama. # ambaye moyo wake umejaa mitego na nyavu Hapa neno "moyo" linamaanisha mawazo na hisia. Huyu ni mwanamke ambaye anajali ya kwake tu. "anayetaka kumtega mtu" # mitego na nyavu Maneno haya mawili yote yanaonesha njia ambazo watu wanatega wanyama. Anaendelea kufikiria njia za kuwatega wanaume ili wampe vitu. # mikono yake ni minyororo Hapa neno "mikono" inamaanisha nguvu au mamlaka ya kuongoza. "ambaye hakuna awazaye kutoroka" # mwenye dhambi atachukuliwa naye "atamkamata mwenye dhambi"