# akizaa watoto mia moja "akizaa watoto 100" # kuishi miaka mingi, ili kwamba siku za miaka yake ni nyingi Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kuleta msisitizo. # moyo wake hautosheki kwa mema "haridhika na vitu vizuri" # hazikwi kwa heshima Maana zinazowezekana ni 1)"hakuna atakayemzika" au 2) "hakuna atakayemzika vizuri" # Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida "mtoto wa hivyo amezaliwa bure" # anapita katika giza Hapa neno "giza" linaweza kumaanisha kati ya dunia ya wafu au kitu ambacho ni kigumu kuelewa. "anakufa bila kuelewa" # jina lake linabaki limefichika "hakuna ajuaye jina lake"