# Tazama "kuwa makini" au "sikiliza" # kile nilichokiona kuwa kizuri kufaaa Hapa maneno "kizuri" na "kufaa" zinamaana moja. Ya pili inakazia maana ya ile ya kwanza. "kile nilichokiona kuwa bora zaidi kufanya." # wakati wa siku za maisha haya ambayo Mungu ametupa "kadri Mungu atakavyo turuhusu kuishi" # wajibu wa mtu Maana zinazowezekana ni 1) "dhawabu ya mtu" au 2) "fungu la mtu maishani"