# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kubariki kabila za Israeli, baraka ni shairi fupi. # Kuhusu Yusufu Hii ina maana ya kabila la Efraimu na kabila la Manase. Kabila zote mbili zilitokana kwa Yusufu. # Nchi yake na ibarikiwe na Yahwe Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na Yahwe abariki nchi yao" # na vitu vya thamani vya mbinguni, na umande "kwa umande wa thamani kutoka mbinguni" au "kwa mvua ya thamani kutoka mbinguni" # umande maji ambayo hujiunda juu ya majani na nyasi katika asubuhi za baridi. # kina kilalacho chini Hii ina maana ya maji chini ya ardhi.