# Taarifa ya Jumla: Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli. # mimi, hata mimi "Mimi, mimi" au "mimi mwenyewe". Yahwe anarudia "mimi" kusisitiza ya kuwa yeye pekee ndiye Mungu. # ninainua mikono yangu mbinguni na kusema "Ninainua mkono wangu mbinguni na kuapa" au "Nimetamka kiapo". Kwa kuinua juu mkono ni ishara ya kutoa kiapo. # Niishivyo milele "Niishivyo milele" au "Ninaapa kwa maisha yangu ambayo hayana mwisho". Kauli hii inawahakikishia watu ya kwamba kile asemacho Mungu katika 32:41-32-42 kitatokea.