# Taarifa ya Jumla: Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli. Huu ni mwisho wa nukuu ya Musa ya maneno ya Yahwe ambayo inaanza katika 32:19. # Kisasi ni changu kutoa, na fidia Maneno "kisasi" na "fidia" kimsingi ina maana moja. "Nitakuwa na kisasi na kuadhibu adui wa Israeli" # fidia kuadhibu au kuzawadia mtu kwa kile alichofanya # mguu wao utakapotereza Jambo baya limefanyika kwao. "hawajiwezi" # siku ya maafa kwao "wakati wangu kuwaangamiza" # na vitu vitakavyokuja juu yao vitaharakisha kutendeka Yahwe anazungumzia kuhusu mambo mabaya yatakayotokea kwa adui zake kana kwamba mambo mabaya walikuwa watu wanaokimbia kwa shauku kuwaadhibu. "na nitawaadhibu haraka"