# Taarifa ya Jumla: Musa anazungumza wimbo wa shairi kwa watu wa Israeli. Anaendelea kutoa nukuu maneno ya Yahwe. # Nje panga litawatwaa Hapa "panga" inawakilisha jeshi la maadui. "Waisraeli wanapokuwa nje, jeshi la adui litawaua" # hofu kuu itafanya hivyo Yahwe anazungumzia kuwa na hofu kana kwamba ilikuwa mtu anayekuja ndani ya nyumba na kuua wale waishio ndani yake. "utakufa kwa sababu unaogopa" # mwanamume kijana na bikra nitawaangamiza, mchanga anyonyaye, na mwanamume mwenye mvi Misemo hii inayoelezea watu wa umri tofauti imeunganishwa kumaanisha ya kuwa kila aina ya watu watakufa. # Nilisema nita ... mbali, kwamba nita ... wanadamu Hii inaweza kutafsiriwa kama nukuu iliyo moja kwa moja. "Nilisema, "nita .. mbali, na nita... binadamu" # nitafanya kumbukumbu yao kukoma miongoni mwa wanadamu "Nitawafanya watu wote kusahau kuhusu wao"