# Habari ya jumla Musa anazungumza kwa Waisraeli kama walikuwa mtu mmoja, hivyo maneno "wewe" na "yako" hapa yako kwenye umoja. # shangwe na furaha moyoni Hapa "shangwe" na "furaha moyoni" umaanisha kitu kile kile. Yanasisitiza kwamba watu wanapaswa kuwa na furaha kumwabudu Yahwe. # Ataweka mzigo wa chuma juu ya shingo yako Huu ni mfano kwa ajili ya Yahwe kumruhusu adui kuwafanyia Waisraeli kwa ukatili na kuwafanya watumwa.