# Habari ya jumla Musa anazungumza na Waisraeli kama walikuwa mtu mmoja, hivyo maneno "wewe" na "yako" hapa yako kwenye umoja. # Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako Hii inaweza kusemwa kwa mfumo kazi. "Utashuhudia mtu fulani anamuawa ng'ombe wako" # punda wako atachukuliwa kwa nguvu mbele yako na hatarejeshwa kwako. Hii inaweza kusemwa kwa mfumo kazi. "mtu fulani atamchukua punda wako kwa nguvu na hatamrudisha" # Kondoo wako watapewa maadui zako Hii inaweza kusemwa kwa mfumo kazi. "Nitawapa kondoo zako maadui wako" au "Nitawaruhusu maadui zako kuchukua kondoo wako"