# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuwaambia Walawi na watu kile wanachopaswa kusema. # Alaaniwe mwanamume Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Na Yahwe alaani mwanamume" # atumiaye nguvu kupokonya haki inayomstahili mgeni ... mjane Musa anazungumzia haki kana kwamba ilikuwa kitu halisia ambayo mtu mwenye nguvu anaweza kuvuta kwa nguvu kutoka kwa mtu dhaifu. Lugha yako inaweza kuwa na neno moja yenye maana "kutumia nguvu kuchukua". Maana zingine zinajitokeza katika 24:17."kumtendea mgeni ... mjane bila haki" # yatima Hawa ni watoto ambao wazazi wake wawili wamefariki na hawana jamaa wa kuwatunza. # mjane Hii ina maana ya mwanamke ambaye mume wake amefariki na hana watoto ambao wanamtunza katika uzee wake.