# Taarifa ya Jumla: Hii inaendeleza kile ambacho Muisraeli anatakiwa kusema pale anapoleta mazao yake ya kwanza kwa Yahwe. # Yahwe alituondoa Hapa "alituondoa" ina maana ya watu wa Israeli ambao walikuwa wakiishi Misri. Mwandishi anajijumlisha mwenyewe kama mmoja wa watu hata kama aliishi Misri au la. # kwa mkono wake mkuu, kwa mkono wake ulionyoshwa Hapa "mkono mkuu" na "mkono ulionyoka" ni sitiari kwa nguvu ya Yahwe. "kwa kuonyesha nguvu yake" Maneno kama haya hujitokeza katika 4:34. # kwa hofu kuu "kwa matendo ambayo yaliwatisha watu waliyoyaona" # nchi inayotiririka kwa maziwa na asali Hii ni lahaja. "nchi yenye maziwa mengi na mtiririko wa asali" au "nchi ambayo inafaa kwa mifugo na ukulima"