# Taarifa ya Jumla: Hii inaendeleza kile Muisraeli anapswa kulema anapoleta mazao yake ya kwanza kwa Yahwe. # walitutendea vibaya na kututesa Misemo hii miwili kimsingi inasema kitu kimoja. Inasisitiza ya kwamba Wamisri walitenda kwa ukatili sana. # walitutendea Hapa "walitutendea" ina maana ya watu wa Israeli ambao walikuwa wakiishi Misri. Mwandishi anajijumuisha mwenyewe kama mmoja wa watu hata kama aliishi Misri au la. # akasikia sauti yetu Hapa "sauti" ina maana ya mtu mzima na kilio au maombi yake. "alisikia vilio vyetu" au "alisikia maombi yetu" # mateso yetu, kazi zetu na mateso yetu "ya kwamba Wamisri walikuwa wakitutesa, ya kwamba tulikuwa tukifanya kazi ngumu sana, na kwamba Wamisri walikuwa wakitutesa"