# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "yako" hapa ni katika umoja. # Utakapovuna zao lako shambani mwako "Utakapokata zao la shamba lako" # tita mazao ambayo mvunaji amezifunga pamoja # kinapaswa kuwa cha mgeni, cha yatima, au cha mjane Unaweza kufanya taarifa ieleweke. "unatakiwa kubakia tita ili kwamba mgeni, na yatima, au mjane anaweza kuchukua" # katika kazi ya mikono yako Hapa "mikono" ina maana ya mtu mzima. "katika kazi yako yote unayofanya" # Utakapotikisa mti wako wa mzeituni Unaweza kufanya taarifa ieleweke. "Unapotikisa matawi ya mti wa mzeituni, kusababisha mzeituni kuanguka kwenye nchi ili uweze kuchukua" # haupaswi kupanda juu ya matawi tena "usiokote kila tawi moja kutoka kwenye mti" # itakuwa kwa ajili ya mgeni, kwa yatima na kwa mjane Unaweza kufanya taarifa ieleweke. "mizeituni inayobaki katika matawi ni kwa ajili ya wageni, yatima, na wajane kuokota na kuondoka navyo"