# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # Mwanamume akimchukua mke na kumuoa Misemo "kuchukua mke" na "kumuoa" ina maana moja. "Mwanamume anapomuoa mwanamke" # asipokubalika machoni pa mumewe Hapa "machoni pake" ina maana ya mtu mzima. "akiamua ya kwamba hampendi" # kwa sababu kagundua jambo ambalo si jema kwake "kwa sababu fulani ameamua ya kwamba hataki kukaa naye" # anatakiwa amwandikie talaka "anapaswa kumpa mke wake karatasi rasmi inayosema ya kwamba hawajoana tena" # anaweza kwenda na kuwa mke wa mwanamume mwingine "anaweza kuondoka na kuolewa na mwanamume mwingine"