# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo neno "wako" hapa ni katika umoja. # Hutakiwi kumkopesha Muisraeli mwenzako kwa riba "Kama utakopesha kitu kwa Muisraeli mwenzako, hautakiwi kumfanya alipe zaidi ya alivyokopa" # kukopesha kwa riba kumkopesha mtu na kumlazimisha mtu huyo kulipa zaidi ya kile alichokopa # riba ya fedha ... kitu chochote kinachokopeshwa kwa riba "hautakiwi kulipiza riba unapomkopesha mtu pesa, chakula, au kitu chochote" # kila jambo uwekalo mkono wako Hii ni lahaja. "kila unachofanya"