# Taarifaya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # na kisha kumtuhumu kwa vitu vya aibu "na kisha kumtuhumu yeye kulala na mtu mwingine kabla hajaolewa" # na kumharibia sifa yake Nomino inayojitegemea ya "sifa" inaweza kutafsiriwa kama msemo wa kitenzi. "na kufanya watu wengine kufikiri kuwa yeye ni mtu mbaya" # lakini nilipomkaribia Hii ni njia ya upole ya kusema "kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu". "lakini nilipolala naye" # sikukuta ushahidi wa ubikira kwake Nomino inayojitegemea ya "ushahidi" inaweza kutafsiriwa kama msemo wa kitenzi. "hakuweza kutoa ushahidi kwangu ya kwamba alikuwa bikira"