# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # wanapaswa kuja mbele "wanapaswa kuja bondeni" # kwa maana Yahwe Mungu wako amewachagua wamtumikie yeye "kwa sababu makuhani ndio wao ambao Yahwe Mungu wako amewachagua kumtumikia" # Yahwe Mungu wako Musa anazungumza na Waisraeli kana kwamba alikuwa akizungumza na mtu mmoja, kwa hiyo neno "wako" ni katika umoja. # kutoa baraka kwa watu "kubariki watu wa Israeli" # katika jina la Yahwe Hapa lugha nyingine "katika jina la" ina maana ya Yahwe na mamlaka yake. "kama yule asemavyo na kufanya kile Yahwe mwenyewe angesema na kufanya" # sikiliza ushauri wao "sikiliza kile makuhani wanachosema" # kwa maana neno lao litakuwa hukumu Hapa lugha nyingine "neno lao" ina maana ya kile makuhani wanachosema. "kwa sababu chochote makuhani wanchosema, huo utakuwa uamuzi wao" # katika kila mtafaruku na ugomvi "kila wakati watu wanapokuwa mahakamani kwa sababu ya kutokuelewana baina yao au mtu kudhuru mtu mwingine"