# Taarifa ya jumla Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli # Lakini ni kwa namna gani mimi peke yangu nibebe shehena zenu, mizigo yenu, na mizozo yenu? Musa anatumia swali kusisitiza kwamba hawezi kutatua shida zao yeye mwenyewe. Swali hili la kejeli linaweza kutofasiriwa kama taarifa. # beba shehena zenu, mizigo yenu Musa anazungumza kama shida za watu na malalamiko aliyohitaji kushughulikia vilikuwa vitu vizito ambavyo alikuwa amebeba. # migogoro yenu "mabishano yenu" au "kutokubaliana kwenu" # watu wa tabia nzuri kutoka kila kabila "watu ambayo watu wa kila kabila la Israeli huwatii"