# Maelezo ya jumla Malaika anaendelea kuongea na Danieli # mmoja kati ya maamiri jeshi wake atakuwa mwenye nguvu kuliko yeye na atautawala ufalme wake kwa nguvu kubwa Kamanda wa mfalme wa Kusini atakuwa Mfalme wa Kaskazini. # watafanya mwungano Mfalme wa Kusini atafanya ushirika na Mfalme wa Kaskazini. Mwungano huu utakuwa wa makubaliano rasmi ambayo kila taifa lazima kuyafuata. # Binti wa mfalme wa Kusini atakuja kwa mfalme wa Kaskazini kuyathibitisha makubaliano yao. Mfalme wa Kusini atampa binti yake mfalme wa kusini ili amwoe. Ndoa itathibitisha makubaliano kati ya wafalme hawa wawili. # nguvu za mkono wake.... mkono wake Mahali hapa "mkono" unatumika kumaanisha nguvu. # Ataachwa Hii inarejelea hila ya kuuliwa kwa binti na wale ambao wamefanya mwungano. Kirai hiki chaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " Watamwacha"