# Yeye aliyekuwa kama wana wa mtu Kauli hii inamrejelea yeye ambaye alikuwa ameongea na Danieli. Ingawa, baadhi ya matoleo hutafsiri kwamba alikuwa anamrejelea mtu mwingine tofauti. # kama wana wa mtu Maelezo haya yanawarejelea watu kwa ujumla # masumbuko mateso makali ya kihisia # Mimi ni mtumishi wako. Je ninawezaje kuongea na Bwana wangu? Danieli anauliza swali hili kumaanisha kwamba yeye hawezi kuongea na malaika kwasababu yeye halingani na malaika. Sentensi hizi zaweza kuunganishwa. "siwezi kukujibu wewe kwasababu mimi ni mtumishi wako" # hakuna pumzi iliyosalia ndani yangu." Nahau hii inarejelea upumuaji. "Siwezi kupumua" au "ni vigumu sana kupumua"