# Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu Hapa "uso" unawakilisha kusudi la Danieli. "Nililielekeza kusudi langu kwa Bwana Mungu" # kumtafuta yeye Wale wanaotaka kumjua Yahweh na kumpendeza Yeye wanasemwa kana kwamba walikuwa wakimtafuta ili kumpata Yahweh. # kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu. Hizi ni ishara za matendo ya toba na huzuni # niliungama dhambi zetu "Nilikiri dhambi zetu" # hutunza maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wanaokupenda "hufanya kile alichokisema angelikifanya katika agano lake na hutunza ahadi zake ili kuwapenda wale"