# Maelezo ya jumla Danieli anaendelea kuelezea maono yake ya mahakama ya mbinguni katika kujibu mnyama wa nne aliyemwona katika 7:6 # mnyama anauliwa...kwa ajili ya kuchomwa moto Kauli hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "walimwua mnyama wa nne, wakaharibu mwili wake na wakampa mtu fulani ili auchome." # mnyama Hii inamrejelea mnyama wa nne ambaye alikuwa na pembe kumi na pembe ile iliyojivuna. # Na kwa wale wanyama wanne waliosalia, Inaweza kuwa wazi kusema, "wanyama wengine watatu" # mamlaka yao yalitwaliwa mbali, Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "hakimu aliyachukua mamlaka yao ya kutawala" au "mamlaka yao ya kutawala yalikoma' # maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. " waliendelea kuishi kwa kipindi fulani cha muda" au "hakimu aliwaacha waishi kidogo"