# walileta mpango mbele ya mfalme "waliwasilisha mpango kwa mfalme" # Mfalme Dario, uishi milele! Hii ilikuwa ni njia ya kawaida ya kumsalimia mfalme. # siku thelathini "kwa siku 30" # mtu yeyote anayefanya dua "yeyote atakayetoa ombi" # mtu huyo lazima atupwe katika tundu la simba Maneno haya yaweza kuelezeka kwa muundo tendaji. "wanajeshi wako lazima wamtupe mtu huyo katika tundu la simba" # tundu la simba Hii inarejelea chumba au shimo mahali ambapo simba walikuwa wametunzwa