# moyo ulipokuwa na kiburi Mahali hapa neno "moyo" linamrejelea mfalme mwenyewe. # roho yake ilifanywa kuwa mgumu Mahali neno "roho" linamaanisha mfalme mwenyewe. Kiburi chake kinasemwa kana kwamba kilikuwa kimefanywa kuwa kigumu. # kwa kiburi "kwa kiburi na zaidi ya kujiamini # alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme Mahali "kiti cha enzi" kina maana ya mamlaka yake ya kutawala. Hii pia yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Watu waliutwaa ufalme wake." # Aliondolewa katika ubinadamu Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. Watu walimfukuza atoke kati yao" # alikuwa na akili za mnyama, Mahali hapa neno "akili" lina maana ya mawazo. "Alifikiri kama vile mnyama anavyofikiri" # umande Ni unyevu nyevu ulio juu ya nchi ambao hupatikana nyakati za asubuhi. # yeyote amtakaye "yeyote amchaguaye"