# Ndipo Danieli alipoletwa mbele ya mfalme Hii yaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. "Kisha walimleta Danieli mbele ya mfalme" au "wanajeshi walimleta Danieli mbele ya mfalme" # ambao baba yangu mfalme aliwaleta kutoka Yuda Katika kirai hiki, neno "baba" limetumika kumaanisha wanajeshi wote. # roho ya miungu Belshaza aliamini kuwa nguvu za Danieli zilitoka kwa miungu ya uongo ambayo Belshaza aliiabudu. # mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "una mwanga na ufahamu na hekima bora"