# Mtu yeyote asiyeanguka na kuiabudu sharti atupwe katika tanuru linalowaka moto Tungo hii yaweza kuelezwa kwa kutumia muundo tendaji. "Wanajeshi watawatupa katika tanuru liwakalo moto mtu yeyote ambaye hatalala chini na kuabudu." # kuanguka chini Hili ni tendo la ishara ya kuabudu # tanuru la moto Hiki ni chumba kikubwa chenye moto mkali # masuala "mambo" au "shughuli" # Shadraka, Meshaki, na Abednego Haya yalikuwa ni majina ya Kibabeli ya vijana watau wa Kiyahudi ambao walikuwa ni marafiki wa Danieli. # hawakutii wewe "hawakusikilizi wewe" # kuisujudia wenyewe Hii ni ishara ya tendo la kuabudu # sanamu ya dhahabu ambayo umeiweka Hii inazungumzia juu ya mfalme Nebukadneza kutoa amri ya kujengwa kwa sanamu kana kwamba yeye mwenyewe aliijenga. "Sanamu uliyowaagiza watu wako waijenge"