# alianguka kifudifudi Tendo hili linaonesha kwamba mfalme alikuwa anamheshimu Danieli. "lala chini huku kichwa kimeelekea chini." # sadaka zitolewe na manukato yatolewe kwake Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Watumishi wake walitoa sadaka na kutoa manukato kwa Danieli." # Hakika Mungu wako "Ni kweli kwamba Mungu wako" # Mungu wa miungu, Bwana wa wafalme, "mkuu kuliko miungu mingine, na mfalme juu ya wafalme wengine wote" # ambaye hufunua mafumbo "yeye ambaye hufunua siri" # kufumbua mafumbo haya "kufunua siri za ndoto yangu"