# Nebukadneza Jina hili humrejelea Nebukadneza na wanajeshi wake, siyo yeye peke yake. # kuzuia mahitaji yake yote "Kuwazuia watu wasipokee mahitaji" # Yehoyakimu mfalme wa Yuda Hii inamrejelea Yehoyakimu na wanajeshi wake, siyo Yehoyakimu peke yake. # alimpatia Yehoyakimu alimpa Nebukadneza # alivipeleka ...aliviweka Ingawa Nebukadneza hakufanya vitu hivi peke yake, ni vizuri kwa msomaji kutumia umoja tu. # Alivipeleka Kiwakilishi 'vi' kinarejelea vitu/vifaa vitakatifu vilivyochukuliwa kutoka Yerusalemu. # hazina ya mungu wake Hiki kitendo kilikuwa na ibada kwa mungu wake