# Sentensi unganishi Paulo anendelea kuwapa maelezo waamini juu ya kuishi na kuongea. # Maelezo kwa jumla: Hapa neno "sisi" linarejea kwa Paulo na Timotheo ila sio Wakolosai. # Endelea kuwa thabiti katika maombi "endelea kuomba kwa uaminifu" au "endelea kuomba mara kwa mara" # Mungu afungue njia "Mungu ataandaa fursa" # siri ya kweli ya Kristo Hii inarejea injili ya Yesu Kristo, ambayo haikueleweka kabla ya kuja Kristo kuja. # Kwa sababu ya lile neno , mimi nilifungwa. Kwa kutangaza ujumbe ule wa Yesu Kristo sasa nimefungwa. # omba ili niweze kusema kwa uwazi "omba niwe na nguvu na uwezo wa kutoa ujumbe wa Yesu Kristo kwa uwazi"