# Sasa neno hili linaweka alama ya kuhama kutoka katika hoja ya Paulo. Hapa anaanza kuelezea hali katika Yerusalemu wakati baadhi ya Wayahudi walipomweka Paulo nguvuni. # baada ya miaka mingi "baada ya miaka mingi kutoka Yerusalemu" # Nilikuja kuleta misaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha Hapa "nilikuja" inaweza kutafsiriwa kama "Nilikwenda." "Nilikwenda kusaidia watu wangu kwa kuwapelekea fedha kama zawadi" # katika sherehe ya utakaso katika hekalu "katika hekalu baada ya kumaliza sherehe ya kujitakasa mwenyewe" # Bila umati wa watu au ghasia Hii yaweza tajwa kama kauli mpya. "Mimi nilikuwa sijakusanya umati wala sikujaribu kuanzisha ghasia" # wamaume hawa "Wayahudi kutoka Asia" # kama wanajambo lolote "Kama wana jambo lolote la kusema"