# Sentensi unganishi Huu ni mwanzo wa sehemu ya hadithi kuhusu kukamatwa kwa Paulo. # Taarifa ya jumla Mstari wa 29 unaelezea habari kuhusu Wayahudi kutoka Asia. # Siku saba Hizi zilikuwa siku saba kwa ajili ya kujitakasa. # katika Hekalu Paulo hakuwa ndani ya hekalu lenyewe. Alikuwa kwenye uwa wa nje wa hekalu. # Makutano wote wakashawishika "Ilisababisha kundi kubwa la watu kuanzisha upinzani. # na wakamnyoshea mikono Neno Kumnyoshea mikono" lina maana ya watu kuanza kumvamia. # watu, sheria na mahali "Watu wa Israel, sheria ya Musa, na hekalu # mwanzoni walikuwa wamemwona...walidhani kwamba Paulo alikuwa ameingia na Myunani hekaluni Mwandishi Luka anaelezea kwanini wayahudi kutoka Asia walimshitaki Paulo kuwa alimleta Myunani # Trofimu Huyu alikuwa mwanaume Myunani ambaye Paulo alishitakiwa kuwa aliingia naye hekalu