# Taarifa ya jumla Fungu hili limawahusu Yakobo na wazee wengine. # watu wanne ambao waliweka kiapo Hii ilikuwa ni aina ya kiapo ambapo mtu hakutaka kunywa kileo au kukata nywele zao mpaka mwisho wa kipindi cha kuweka muda. "watu wanne ambao walitoa ahadi kwa Mungu." # Wachukue watu hawa na ujitakase mwenyewe pamoja nao Walikuwa wanapaswa wao wenyewe kujitakasa ili waweze kuabudu ndani ya hekalu. # na uwalipie gharama zao Lipa kile ambacho watahitaji kulipiwa. # ili waweze kunyoa vichwa vyao Hii ni ishara ya mtu anayetimiza nadhili yake kwa Mungu. # mambo waliyoambiwa kuhusu wewe Mambo ambayo yanasemwa na watu kukuhusu wewe. # Kufuata sheria Inamaanisha utii wa kuzishika sheria za Mungu.