# Sentensi unganishi Paulo anaanza rariba yake akiwa Kaisaria # tuliwasili Tolemai Tolemai ulikuwa ni mji wa kusini mwa Tiro, Lebanoni. Tolemai ya sasa ni Acre, Israeli. # ndugu hawa "waumini wenzake" # mmoja kati ya saba "Saba" inahusu wanaume waliochaguliwa kusambaza chakula na misaada kwa wajane. # mtu huyu "Philipo" # Sasa Neno hili limetumika kama alama ya kumalizika kwa tukio moja na kuanza kwa tukio jingine. Luka anasimulia habari za Philipo na binti zake. # mabinti wanne mabikira ambao walitabiri "Mabinti bikra wanne ambao kwa kawaida walikuwa wakipokea na kupeleka ujumbe kwa watu kutoka kwa Mungu.