# Taarifa unganishi Paulo anawaita wazee wa kanisa la Efeso na kuanza kuzungumza nao. # kutoka Mileto Mileto ilikuwa ni mji wenye bandari Magharibi ya Asia ndogo karibu na chanzo cha mto Meander. # Ninyi wenyewe Paulo hapa anatumia msisitizo kwa kile anachowaambia. # kuweka mguu katika Asia aliingia mkoa huu wa Asia # jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote Anazungumzia muda alioutumia akiwa kwao. # kwa unyenyekevu wote 'Unyenyekevu' au 'kujishusha hadi chini' # kwa machozi "machozi" wakati mwingine alijisikia hali ya huzuni na kulia machozi. # kwa Wayahudi Hii haimaanishi kwa kila Myahudi. Anaelezea juu ya baadhi ya wale waliomtendea mabaya. # Mwajua jinsi ambavyo sikujizuia kutangaza kwenu " Mnajua jinsi ambavyo sikunyamaza, lakini kila mara niliwahutubia." # kwenda nyumba kwa nyumba Paulo alifundisha watu kwenye makazi yao binafsi yaani nyumba kwa nyumba. # juu ya toba kwa Mungu na imani katika Bwana wetu Yesu "toba" na "imani" ni maneno yanayoweza kutafsiriwa kwa vitenzi. Kwamba walipaswa kutubu mbele za Mungu na kuamini katika Bwana Yesu Kristo.